Shairi: Chaurembo

Shairi: Chaurembo

Shairi: Chaurembo

Na: Kassim Kombe

Kwa uzuri wako na maumbile yako,

Si wanaona gere mabinti wenzako,

Ewee chaurembo hivi ana fikra za kuwa mpinzani wako…,

Vijana kwa wakongwe umetunasa kama sumaku, si maneno ya kanga wala udaku…. mie niko mstari wa mbele shabiki wako,

Hivi wee chaurembo ulizaliwa majira gani…., manake uzuri wako si wa kawaida hapa duniani,

Sitokufuru nikiamba wewe ni malaika wa peponi… Nurulaini.

 Chaurembo…., jina lafanana na wewe… hili taji la urembo ni lako mwenyewe…

Zama nenda zama rudi…, uzuri wako ewee Chaurembo utahadithiwa,

Sifa nzuri unazo wewe zakusifiwa…

Huna dosari kamwe yakukashifiwa.,

Aaaaah Chaurembo …jina lafanana na wewe, hili taji la urembo ni lako mwenyewe…,

Mie malenga mpambe mashairi chungu nzima nakutungia,

Ikibidi niwe Masauti, nyimbo ainati nitakuimbia…,

Au hata Wallah bin Wallah, vitabu vya lugha na fasihi ewee Chaurembo nitakuandikia..,

Weee Chaurembo uzuri wako si wa kudhania kama nomino za dhahania…,

Muonekano wako tu…moyo wangu hutweta kupasua kidari…,

Chaurembo umegonga vichwa vya habari…, simulizi za kina Jeff Koinange, Victoria Rubadiri…yaani uko midomoni mwa wanahabari…,

Una mvuto wa ajabu…, ulorithi kutoka nyanya na babu,

Asili yako mchanganyiko wa kibajuni na kiarabu,

Chaurembo…jina lafanana wewe, hili taji la urembo ni lako mwenyewe…,

Mikono juu nimeshasalimu amri…,

Swadakta mfano wa iliki kukolea kwenye mahamri,

Sura yako cinderella mdoli,

Macho yako ya Vanessa mdee eeeh ya gololi…,

MashaAllah vishimo vimetokea mashavuni…, hayo manukato unayojirashia natamani uwe nami ubavuni…,

Chaurembo, hili taji la urembo ni lako mwenyewe,

Tabasamu lako la geresha…,

Sivyo mabarobaro hushikwa na presha pia matumbo ya kuendesha..

Hilo umbo lako la nambari nane..,

Kidogo wewe na Wema Sepetu  mufanane…,

Mwana wewe umejazajaza buibui…, ukitembea nazi nazi tui tui,

Chaurembo…, hili taji la urembo ni lako mwenyewe…

#CHAUREMBO#

Mwandishi: Kassim Kombe almaarufu malenga_mpambe

Email: kassimkombe@gmail.com

Avatar

admin

leave a comment